MKE wa Mbunge wa Lupa (Chunya) Mkoani Mbeya Bi Veronica Masache Kasaka akishirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya DIDO MWANAFUNZI INITIATIVE wameshiri katika kugawa Sare za Shule kwa watoto wenye uhitaji maalumu katika shule ya msingi Kibaoni.

Mbali na sare za shule, pia amegawa Taulo za kike kwa mabinti wenye umri stahiki.

Zoezi hili limefanyika pia katika Shule ya Sekondari Itewe pamoja na Secondari ya Makala.




akizungumza na  walimu pamoja na wanafunzi Mke wa Mbunge amewajuza walimu na wanafunzi kuwa kupitia ofisi ya Mbunge jimbo la Lupa (Chunya) Wataendelea kutafuta na kuziomba Taasisi zingine ili kusaidia kuwafikia wanafunzi wengi zaidi katika shule nyingine zilizopo Wilayani Chunya.