Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mbeya Mhe. Suma Ikenda Fyandomo, amekabidhi msaada wa kitanda cha kujifungulia pamoja na mashuka ya wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Rungwe (Makandana) Mkoani Mbeya.
Wakati akiwa katika zoezi la kukabidhi kitanda na mashuka amekutana na mwananchi ambaye ni jirani yake katika Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Ndugu Seleman Ismael na mkewe wakiwa wamejaliwa mapacha watatu, wa kike mmoja na wakiume ambao ni miongoni mwa watoto kumi waliozaliwa usiku wa kuamkia Juni 14 2023
"Hakika Mungu ni mwema nimekuja kutoa masaada lakini imekuwa bahati nimekutana na jirani yangu amejaliwa watoto mapacha watatu" amesema Sema Ikenda Fyandomo
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mbunge huyo amesema ametoa vifaa kwa lengo la kuunga juhudi za Serikali chini na Rais Samia Saluhu kutatua changamoto za wananchi ikiwemo Sekta ya Afya.
0 Comments