MBUNGE wa Jimbo la Lupa (Chunya) Mhe. Masache Njelu Kasaka amekutana na Wazee wa Chunya mjini mara baada ya vikao vya Bunge la Bajeti kuhitimishwa hivi karibuni Mjini Dodoma.

Amesema lengo la kukutana na wazee hao ni kuwapa mrejesho wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi 2020-2025 pamoja na kuchukua changamoto zinazowakabili wazee, Jamii na wilaya ya Chunya.


Mbunge huyo aliambatana na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Ndugu Ilomo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chunya Comrade Charles Jokel, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu Kambona